Thursday, 24 May 2018

CCM YAITISHA MKUTANO WA KAMATI KUU NA NEC JIJINI DAR ES SALAAM.


Chama cha Mapinduzi-CCM kimetangaza kufanya vikao vyake vya uongozi vya kitaifa ikiwemo cha Kamati Kuu-CC  na Halmashauri Kuu ya Taifa-NEC kuanzia Mei 28 hadi 29, 2018 jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa mapema leo Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM ambayo iko chini.

MEYA MWITA KUNOGESHA FAINALI ZA PAMBANO LA NGUMI KESHO

MPAMBANO wa shindano la kombe la ngumi la Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita limeendelea kushika kasi kabla ya kuingia fainali hapo kesho.

Jula ya  mabondia 36 wataingia uliongoni leo kupimana nguvu katika uwanja wa ndani wa Taifa kutafuta mabondia 20 watakao ingia kwenye fainali hapo kesho.


Mchuano huo wa aina yake hapo kesho utashuhudiwa na Meya Mwita na wananchi wa jijini hapa ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya kombe,huku mshindi wa pili kwa kila uzito atapata medali za dhahabu.

Aidha mshindi wa tatu kwa kila uzito atapatiwa zawadi ya medali za fedha ambapo zawadi hizo zitatolewa kwa washindi na Meya Mwita.

Mwisho.

Imetolewa leo ,Mei 24 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.

WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUTOROKA HOSPITALI KWENDA KANISANI KUOMBEWA WAPONE EBOLA


Watu wawili walioathirika na virusi vya ugonjwa wa ebola nchini Demokrasia ya Congo wamefariki dunia baada ya kukimbilia kanisani kuombea badala ya kuwahi hospitalini.

Shirika la Afrika Duniani-WHO limethibitisha taarifa hizo, na kuripoti kwamba marehemu hao walitoroka katika kituo cha matibabu nchini humo na kupelekwa kanisani na ndugu zao kwa lengo la kuombewa maradhi yao.

Afisa wa shirika la WHO Eugéne Kabambi amesema ndugu wa wagonjwa hao walifika katika kituo cha matibabu chini ya shirika la madaktari wasio na mipaka na wakadai kuwachukua wagonjwa wao kwenye kuombewa kanisa.

Wahudumu wa afya nchini DRC wana wasiwasi kwamba huenda ugonjwa huo ukaenea kwa kasi,kufuatia eneo hilo la Mbandaka kuwa na idadi kubwa ya watu wapatao milioni moja.
Shirika la WHO linasema visa 58 vya Ebola vimetokea tangu mei nane mwaka huu ulipotokea mlipuko wa ugonjwa huo.

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULAWITI WATOTO 3

Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti.

Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka.

Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama katika eneo la Nambonde.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwepo baada ya mtuhumiwa kukamatwa kwa masikitiko makubwa wameiomba serikali ichukue hatua kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

KOREA KASKAZINI YAIONYESHEA UBABE MAREKANI, YASEMA HAIWEZI KUACHANA NA MPANGO WA NYUKLIA


Korea Kaskazini imesema haiwezi kuibembeleza Marekani kuhusu mazungumzo baina ya mataifa hayo mawili yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu.

Kiongozi mwandamizi wa Korea Kaskazini, Choe Son-hui amenukuliwa akimtuhumu Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence kwamba ni mjinga, huku akitishia kuwa iwapo mazungumzo hayo yasipofanyika kutakuwepo maonyesho ya ubabe wa nyuklia.


Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kwamba mkutano huo unaweza kuahirishwa au kufutwa kabisa.

Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia.

Friday, 15 April 2016

Simba yathibitisha kushiriki kombe la Nile Basib Club Championship

Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.
Mashindano ya vilabu Kombe la Nile Basin huandailiwa na CECAFA kwa kushirikisha vilabu vilivyoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi kwa nchi wanachama wa CECAFA.
Kocha wa Klabu ya Simba Jackson Mayanja (Katikati), kushoto ni Msemaji wa TFF Baraka Kizuguto.
Bingwa michuano ya kombe hilo atajinyakulia zawadi ya dola za kimarekani U$30,000, mshindi wa pili dola U$20,000, huku mshindi wa tatu akipata kitita cha dola za kimarekani U$10,000.
Nile Basin inashirikisha vilabu kutoka katika nchi wanachama wa CECAFA ambazo ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Zanzibar.
Vitoria University kutoka Uganda ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika mwaka 2014.

Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza na kuzifunga Kliniki mbili

Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla (Kulia).

Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amezifunga kiliniki mbili za Kikorea zinazotoa huduma ya tiba asili nchini kwa kosa la kutoa huduma bila ya kuwa na kibali pamoja na kuchanganya tiba asili, mbadala na ya kisasa pasipo Wizara ya Afya kuthibitisha kama vifaa inavyotumia vina ubora.
Aidha, Kliniki hizo zenye majina ya Korea Medical Clinic na Maibong Ukidar Medical zilizopo jijini Dar es Salaam zinatuhumiwa kutibu magonjwa ambayo katika usajili wake hayapo huku moja  ikitumia jina la CCM kama kinga ya kutofungiwa jambo lililopingwa vikali na Kigwangalla.
"Acha kusingizia kuwa kliniki yako ina uhusiano na CCM, usiichafue kwa kuwa haiko hivyo. Mimi mwenyewe ni mwanaccm sijapendezewa na kauli yako na ninakuagiza ulithibitishie baraza la tiba asili mmiliki halali wa kliniki hii na uache kutumia jina la CCM," amesema Kigwangalla.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kliniki hizo, Kigwangalla ametoa agizo kwa Baraza la Usajili Tiba Asili nchini kuandika barua za kuzifunga kliniki hizo huku akimtaka msajili wa hospitali binafsi kufanya uchunguzi wa vifaa vinavyotumika katika kliniki hizo.