Friday 25 July 2014

Wawili wakamatwa na viungo vya binadamu



Wafanya biashara wawili mashughuri  kwa  kuuza viungo vya binadamu  nchini Nigeria wakamatwa,watuhumiwa hao walikutwa na viungo vya binadamu ikiwemo kichwa,miguu,na mkono katika kijiji cha Tabira nchini Nigeria.
watuhumiwa wakiwa na baadhi ya viungo vya binadamu
Kamishina wa kituo kikuu cha polisi kijijini hapo alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na viungo vya binadamu ambavyo huwauzia wanasiasa wakubwa nchini humo.
Amos Kareem na Abubakar Ladan ndiyo watuhumiwa wanaoshikiriwa hadi sasa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi juu ya njia walizozitumia kupata viungo hivyo.
Aidha jeshi la polisi limedai kuwa watu wengi wamepotea kwa njia za kutatanisha hivyo basi watuhumiwa hao hawataachiliwa hadi watakapo toa ukweli juu ya wahusika wanaofanya nao biashara hiyo haramu ya kuuza viungo vya binadamu.
Mtuhumiwa mmoja anaye fahamika kwa jina la Abubakar Ladan alisema kwamba mtuhumiwa mwenzie Amos Kareem alimuahidi pikipiki endapo atamletea kichwa cha binadamu,ndipo mtuhumiwa huyo alipoamua kwenda makaburini na kufukua kaburi na kufanikiwa kupata viungo hivyo.
Inasadikika kwamba wanunuzi wakuu wa viungo hivyo vya binadamu ni wanasiasa maarufu nchini humo.

No comments: