Vyombo vya habari nchini Morocco vinasema kuwa serikali ya taifa hilo
imeomba kinyang'anyiro cha kuwania kombe la klabu bingwa barani Afrika
cha mwaka ujao kuahirishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola.
Maiti ya Mgonjwa wa Ebola ikienda kuhifadhiwa na wahudumu |
Hatua
hiyo iliafikiwa kutokana na pendekezo la wizara ya afya ambayo inataka
kuyazuia mataifa ambayo yameathiriwa na ugonjwa huo.
Maafisa
nchini Moroco watafanya mazungumzo kuhusu ombi hilo na waandalizi wake
ambacho ni chama cha kandanda barani afrika CAF wiki ijayo.
Mechi
za kufuzu zinazoshirikisha nchi mbili ambazo zimeathiriwa na ugonjwa wa
ebola ambazo ni Guinea na Liberia tayari zimehamishwa ikiwamo mechi
ambayo ilitarajiwa kuchezwa leo .
No comments:
Post a Comment