Thursday 24 May 2018

WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUTOROKA HOSPITALI KWENDA KANISANI KUOMBEWA WAPONE EBOLA


Watu wawili walioathirika na virusi vya ugonjwa wa ebola nchini Demokrasia ya Congo wamefariki dunia baada ya kukimbilia kanisani kuombea badala ya kuwahi hospitalini.

Shirika la Afrika Duniani-WHO limethibitisha taarifa hizo, na kuripoti kwamba marehemu hao walitoroka katika kituo cha matibabu nchini humo na kupelekwa kanisani na ndugu zao kwa lengo la kuombewa maradhi yao.

Afisa wa shirika la WHO Eugéne Kabambi amesema ndugu wa wagonjwa hao walifika katika kituo cha matibabu chini ya shirika la madaktari wasio na mipaka na wakadai kuwachukua wagonjwa wao kwenye kuombewa kanisa.

Wahudumu wa afya nchini DRC wana wasiwasi kwamba huenda ugonjwa huo ukaenea kwa kasi,kufuatia eneo hilo la Mbandaka kuwa na idadi kubwa ya watu wapatao milioni moja.
Shirika la WHO linasema visa 58 vya Ebola vimetokea tangu mei nane mwaka huu ulipotokea mlipuko wa ugonjwa huo.

No comments: