Thursday, 24 May 2018

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULAWITI WATOTO 3

Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti.

Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka.

Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama katika eneo la Nambonde.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwepo baada ya mtuhumiwa kukamatwa kwa masikitiko makubwa wameiomba serikali ichukue hatua kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

No comments: