Wednesday, 23 July 2014

Rais wa Nigeria aahidi kuwakomboa wasichana wa Chibok



Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema serikali yake itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba wasichana  zaidi ya 200 wa shule ya Chibok waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo la Boko Haram mwezi April mwaka huu watakombolewa.
Wasichana zaidi ya 200 walio mikononi mwa Boko Haram
Rais Jonathan alitoa ahadi hiyo wakati alipokutana na wazazi wa wasichana hao jana,Rais huyo amekuwa katika wakati mgumu baada ya kukosolewa na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wake na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu duniani kutokana na kuchelewa kwake kuwakomboa wasichana hao.
Hapo awali wazazi wa wasichana hao waligoma kukutana na Rais Goodluck Jonathan lakini baada ya kupokea ushauri kutoka kwa watu mbali mbali wanaoshughurikia haki za binadamu walikubali ombi la Rais huyo na kukutana naye jana kwa maongezi zaidi.
Ndugu na jamaa wa wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram
Kundi la wanamgambo wa Boko Haram walitoa sharti kali kwa Rais huyo na kumataka awaachie huru wafuasi wa kundi hilo waliokamatwa na jeshi lake,lakini Rais huyo ameonekana kukaidi sharti hilo.
Kitendo cha serikali ya Nigeria kushindwa kutoa msaada kwa wasichana hao hadi sasa kumesababisha wananchi wa nchi hiyo pamoja na waalimu kuandaa kampeni inayofahamika kwa “Bring Back Our girls” ambayo iliungwa mkono na watu wengi mashughuri.
Boko Haram wapo tayari kuwa acha huru wasichana hao endapo Rais Jonathan atatekeleza sharti lao.

No comments: