Korea Kaskazini imesema haiwezi kuibembeleza Marekani kuhusu
mazungumzo baina ya mataifa hayo mawili yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni
mwaka huu.
Kiongozi mwandamizi wa Korea Kaskazini, Choe Son-hui
amenukuliwa akimtuhumu Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence kwamba ni mjinga,
huku akitishia kuwa iwapo mazungumzo hayo yasipofanyika kutakuwepo maonyesho ya
ubabe wa nyuklia.
Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kwamba
mkutano huo unaweza kuahirishwa au kufutwa kabisa.
Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria
mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha
za nyuklia.
No comments:
Post a Comment