Monday, 11 August 2014

Tofauti za kidini bado kikwazo Iraq



Marekani yaendeleza mashambulizi ya anga Iraq,huku Uingereza ikiahidi kutoa msaada wa kijeshi kwa Wakrudi.
Marekani inaendelea kufanya mashambulizi ya anga kaskazini mwa  Iraq, lengo la Marekani kuendeleza mashambulizi ya anga Iraq ni kupambana na kundi la wapiganaji wa kiislam linalofahamika kama Jihadi .
Marekani imezidi kuongeza wanajeshi ili kutoa msaada kwa Wakrudi waishio mji wa Erbil ambao wako kwenye mapambano dhidi ya wapiganaji hao wa kiislam.
Wapiganaji wa jeshi la Wakrudi
Licha ya hivyo bado kundi la wapiganaji wa kiislam wanazidi kuimarisha ngome yao katika eneo hilo,pia kuiteka ngome kubwa ya Iraq katika mji wa Mosul.
Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Sunni waliokuwa wamejificha katika milima iliyo eneo la wakimbizi la Yazid ili kuzuia wapiganaji hao wasiendelee kufanya njama za mashambulizi.
Licha ya Marekani kutoa msaada kwa Wakrudi, Uingereza nayo imeahidi kuendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Wakrudi.Ofisa wazamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Alistair Burt ame
sema nchi hiyo inaweza kusaidia jeshi la Wakrudi ili kupambana na kundi hilo la wapiganaji wa kiislam.
Mgogoro baina ya Wakrudi na kundi la wapiganaji wa Kiislam umesababishwa na tofauti za kidini ambapo kundi hilo la Jihad huwalazimisha maelfu ya watu  waishio nchini Iraq kufuata itikadi za dini ya kiislam .
Nae papa Francis ametoa wito kwa dunia kukomesha uhalifu huo unaoendelea kufanywa nchini Iraq na kuwataka watu waache kubaguana kutokana na tofauti za kidini,alisema maneno hayo wakati wa ibada iliyofanyika siku ya jumapili iliyo pita.

No comments: