Spika wa bunge la Niger Hama Amadou ametoroka nchini kwao
baada ya kamati ya bunge hilo kuafikia kukamatwa kwake kuhusiana na kashfa ya
kuwauza watoto nje ya nchi.
Licha ya kashfa hiyo mtuhumiwa Hama Amadou alidai kuwa kashfa
hiyo si ya kweli na imechochewa na tofauti za kisiasa hasa katika kipindi hiki
alichotangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais mwaka 2016.
![]() |
Spika wa bunge la Niger Hama Amadou |
Aidha mke wa pili
spika huyo na watu wengine 16 walikamatwa mwezi Juni baada ya kutuhumiwa
kuwauza watoto wachanga kusini mashariki mwa Nigeria,watoto hao huuzwa kwa
gharama kubwa yapata maelfu ya dola za kimarekani kwa kila mtoto.
Vyombo vya habari nchini Niger vimeeleza kuwa kesi hiyo
imetoa fursa tosha kwa chama tawala kumuondoa Bwana Amadou kutoka katika chama
hicho.
Kamati kuu ya bunge la Taifa ambalo linajumuisha naibu spika
na wakuu wengine walikutana jumatano na kukubaliana kuwa polisi wanaweza
kumkamata na kumhoji bwana Amadou kuhusiana na tuhuma hizo.
Inadaiwa hadi sasa watoto 30 wameuzwa katika hii
inayohusishwa na utengenezwaji wa stakabadhi bandia na kubadili vyeti vya
kuzaliwa vya watoto waliouzwa.
No comments:
Post a Comment