Kiongozi wa juu wa kundi la Hamas amesema kuwa kuna
uwezekano mdogo wa mazungumzo ya kuleta amani Gaza kufanikiwa kutatua mgogoro
kutokana nahali ya kutoelewana kwa wajumbe waliohudhuria mkutano huo mjini Cairo.
Kiongozi huyo aliyasema hayo katika mkutano mjini Cairo
ambao ulihusisha wajumbe mbali mbali toka Misri,Ezzat AL-rishq ambaye ni mmoja
kati ya wajumbe kutoka Palestina ambaye
aliteuliwa katika mkutano huo aliliambia shirika la habari la AFP kuwa nafasi
ya mapatano kati yao ni ndogo sana.
Naye waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu amesema
wawakilishi wake waliondoka Misri tangu ijumaa na hawatarejea ikiwa maroketi yataendelea
kurushwa Israel na wapalestina.
Hadi sasa hali ya Gaza si shwari,maafisa mjini Gaza wanasema
hivi leo kuna mwanamke ameuawa na watu wengine nane wa familia yake
wamejeruhiwa baada ya kombora kutoka Israel kuipiga nyumba yao iliyo kusini mwa
mji wa Bani Suheila.
Mtu mwengine mmoja aliuawa katika kambi ya wakimbizi wa
kipalestina ya Jabaliya.Hadi sasa wapalestina 1,900 wamepoteza maisha kati ya
hao robo ya idadi yao walikuwa watoto.
No comments:
Post a Comment