Baaba ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane,Alshababi lamtangaza kiongozi mpya.

Wapiganaji wa Alshabaab
Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limethibitisha kuwa kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani.
Ripoti zinasema kuwa kundi la Alshabaab limemchagua kiongozi mpya Ahmad Omar,katika mkutano uliofanyika katika eneo lisilojulikana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema kuwa kiongozi huyo bado hafahamiki vyema.
No comments:
Post a Comment