Msanii maarufu kutoka nchini Nigeria David Adeleke Adedeji(Davido)
anayetamba hivi sasa na nyimbo ya SKELEWU,TCHELETE aliye shirikisha kundi
matata toka nchini South Afrika maarufu kama Mafikizolo hivi karibu alifunguka
na kusema kuwa kutokana na umaarufu alio nao haogopi skendo tena.
Licha ya nyimbo hizo zinazozidi kumpa umaarufu bado msanii
huyu anaongoza kwa kuwa na uwezo wa kufanya show 19 kwa mwezi kutokana na
mashabiki aliofanikiwa kuwa nao Afrika na nje ya Afrika.
Davido amepata tuzo tofauti kama BET International Award,MTV
MAMA,Kora Award,Channel O Music Video
Award,Ghana Music Award,Nigeria Music Award n.k zilimfanya azidi kuwa kivutio
kwa wadau wa muziki duniani.
![]() |
Davido |
Davido alisema maneno hayo kwamba haogopi tena skendo
zinazo sababishwa na umaarufu aliokuwa nao sasa katika mahojiano yaliyofanywa na
chombo cha habari nchini Nigeria kinachofahamika kwa jina la Nigeriacamera.
Hivi karibuni msanii huyu alipata skendo ya kumnyanyapaa
msanii mwenzake Wizkid wakati akifanya show nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment