Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Liberia wapo kwenye
wakati mgumu wa kusitisha maandamo ya wananchi nchini Liberia,wananchi
wanaandama ili wajue hatima ya serikali juu ya kutokomeza janga hili la Ebola.
Licha ya hivyo wananchi hao lengo lao halikufanikiwa baada
ya serikali hiyo kuamuru askari wanashughurika na ghasia kusitisha mara moja
maandamano hayo.
![]() |
Polisi akizuia wananchi wanao andamana katika barabara kuu nchini Liberia |
Waandamanaji hao wenye hasira kali waliweka vizuizi katika
barabara kuu na kusema kuwa serikali inakawia kuchukua miili ya waathiriwa wa
ugonjwa wa Ebola jambo ambalo linahatarisha maisha yao kutokana na usaambaji wa
ugonjwa huo.
Mbaya zaidi shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa
ugonjwa huo wa dhararu ulio hatari unaweza ukadumu katika kipindi cha miongo minne.
Hadi sasa nchi zinazopakana na Liberia,GUINEA Sierra Leone zimefunga
mpaka huku Nigeria ikitoa wito kwa watu kujitolea kusaidia kusitisha ueneaji wa
ugonjwa wa Ebola.
No comments:
Post a Comment