Thursday, 17 July 2014

TGNP yawataka wanawake wasiwe nyuma katika marekebisho ya katiba

Shirika lisilo la kiserikali linaloshughurika na masuala kijinsia na haki za watoto Tanzania TGNP iliwataka wanawake wasibaki nyuma katika marekebisho ya katiba.
Maneno hayo yalisemwa jana katika kongamano lilofanyika makao makuu ya TGNP yaliyopo mabibo jijini Dsm,kongamano hilo lili husisha wanawake kutoka sehemu mbali mbali lengo ni kutoa elimu kwa wanawake ili waweze kutetea haki zao za msingi katika marekebisho ya katiba mpya.
Kwa mujibu wa shirika hilo walidai kuwa unyanyasaji wa kijinsia unazidi shika kasi kutokana na udhaifu wa katiba,endapo kama katiba haitarekebisha mapungufu yaliyopo katika ibara kadhaa itazidi kuchochea unyanyasaji wa jinsia hasa kwa wanawake na watoto.
Wanawake wakiwa katika semina
Wanawake hao waliitaka serikali iweke mkazo juu ya wavulana ama wanaume wanaowapa ujauzito wanafunzi shuleni wachukuliwe hatua za kisheria badala ya kuwafukuza wasichana wajawazito shule.
Kitendo cha kuwafukuza wasichana wajawazito shule kinazidi kuwapa kichwa wanaume wengi hivyo basi kama katiba haitaweka kifungu kitakachohusika na swala hili tatizo hili halitakoma.
Pia waliitaka katiba mpya iunde chombo maalum kitakachowajibisha serikali na taasis mbali mbali nchini katika kutekeleza haki za wanawake kwenye maeneo yote ya kijamii,kisiasa na kiuchumi nchini.
Pia waliitaka katiba mpya ibainishe haki za wanawake,shirika hilo lilitoa semina fupi pamoja na vipeperushi vilivyoandikwa baadhi ya ibara zilizopo katika katiba ya zamani ambazo zinatakiwa zifanyiwe marekebisho.

No comments: