Thursday, 17 July 2014

Muigizaji wa Marekani jela kwa kumtumia Obama barua yenye sumu



Muigizaji maarufu aliyecheza filamu ya The Vampire Diaries na The Walking Death nchini Marekani maarufu kama Shannon Richardson(36) anatuhumiwa kwa kutuma barua tatu zilizobeba sumu,moja kati ya barua hizo alimtumia Rais wa nchi hiyo Barrack Obama na nyingine alimtumia meya wa New York Michael Bloomburg.
Mtuhumiwa Shannon Richardson akijibu mashitaka kizimbani
Baada ya kuulizwa kisa kilichopelekea kufanya tukio hilo alidai kuwa ilikuwa ni kisasi ambapo mumewe aliye achana naye ndiyo aliyemtumia barua hizo.
“Sikuwa na nia ya kumdhuru mtu” Shannon aliiambia mahakama.
Muigizaji huyo alipewa adhabu kubwa ukilinganisha na kosa alilolifanya pia alitakiwa kulipa faini ya dola 367,000.
Shannon  mama wa watoto sita aliagiza bidhaa za kutengeneza sumu hiyo kupitia kwenye mtandao,alitumia bidhaa hizo kutengeneza sumu kisha akatuma barua tatu zilizokuwa zimepakwa sumu hiyo.
Baada ya uchunguzi huo ulipothibitishwa mtuhumiwa alikiri kosa na kudai kuwa ni kweli aliagiza bidhaa alizozitumia kutengenezea sumu kwa kutumia barua ili watu wasigundue mapema lengo lake,licha ya hivyo mpango wake ulikwama baada ya wataalam kuzichunguza barua hizo na kubaini kuwa barua hazikuwa na usalama.
Kulingana na maelezo yaliyotoka kwa washitaki barua aliyotumiwa Obama ilikuwa na maandishi haya,Kilicho ndani ya barua hii hakiwezi kulinganishwa na mipango yangu kwako bwana Rais.
Chanzo kilichopelekea mwana mama huyo afanye uhalifu huo ni baada ya serikali ya Marekani kupinga matumizi ya kiholela ya silaha za moto(Bunduki) ndipo alipoamua kuaandaa barua hizo zenye sumu kwa wahusika.
Barua ya pili iliyokwenda kwa meya wa Bloomberg ambaye anaunga mkono kudhibitiwa kwa bunduki ilisema “Mpige risasi mtu yeyote atakaye kuja kuchukua bunduki za mtu aliyetuma barua hii.”
Barua ya tatu ilisomwa na bwana Mark Glaze mkurugenzi mkuu wa idara inayofadhiliwa na meya ya kupambana na silaha haramu.
Mtuhumiwa akiwa na huzuni baada ya kupokea hukumu
Mtuhumiwa huyo aliiomba mahakama imsamehe sababu lengo lake halikuwa na kumdhuru mtu yeyote,Huku akiwa mwenye huzuni alisema kwamba kitendo cha kunyang’anywa watoto wake sita anahisi ameadhibiwa vya kutosha.

No comments: