Hadi sasa maelfu ya watu nchini Nigeria wamepoteza maisha huku
wengi wao wakibaki hawana makazi ya kudumu wakati wengine wakipata hasara
kutokana na uharibifu wa mali zao.
Nyumba iliyoharibiwa na Boko Haram |
Janga hili limeletwa na kundi linalofahamika kwa jina la
Boko Haram linalotumia itikadi za kidini kuleta mapambano zidi ya serikali ya
Goodluck Jonathan,kundi hilo linaishinikiza serikali ya Rais Goodluck Jonathan
kuwaachilia huru wafuasi wao ambao walikamatwa na jeshi la polisi nchini humo.
Viongozi wa Boko Haram |
Licha ya watu waliopoteza maisha kutokana na milipuko mbali
mbali iliyotokea na utekwaji nyara wa wasichana 200 wa shule ya Chibok Girls nchini humo bado jamii inahuzuni kubwa sababu
hadi sasa haijatambua hatima ya kundi hilo.
Viongozi wa dini ya kiislam nchini Nigeria bado wanapinga
vikali kauli inayotolewa na baadhi ya wananchi wa Nigeria kwamba kundi hilo
linavuruga amani kwa sababu za kidini,viongozi hao wamedai kuwa hakuna dini
inayoruhusu kuanzisha vita visivyo na sababu za msingi.
Hivyo basi kundi hilo liache kuchanganya dini na mambo
wanayoyafanya sababu hata viongozi wa dini ya kiislam nchini humo hawana
mahusiano yoyote na kundi hilo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Nigeria vimedai kuwa
kundi hilo liliundwa rasmi mwaka 2002,lengo la kundi hilo ni kupinga elimu ya kimagharibi.Lilianza
kufanya mashambulizi mwaka 2009.
Kundi hilo limepelekea maelfu ya wanigeria kupoteza maisha
kaskazini mashariki mwa Nigeria,licha ya vifo hivyo kundi hilo lilifanya
mashambulizi makao makuu ya UN mjini Abuja na kusababisha takribani watu milioni
3 kuathirika.
Mali zilizoharibiwa na Boko Haram |
Kundi hilo lilitanganzwa rasmi kuwa ni la kigaidi na nchi ya Marekani
mwaka 2013
Shirika la kimataifa linalo tetea haki za binadamu Human
Rights Watch linasema kuwa zaidi ya raia 2,000 wameuawa nchini Nigeria mwaka
huu na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa shirika hilo vifo hivyo vimetokea katika
mashambulizi 95 tofauti katika miji zaidi ya 70 pamoja na vijiji vilivyopo
mashariki mwa taifa hilo.
Bado maswali yanazidi kuzuka juu ya mfadhili wa kundi hili
haramu sababu mambo wanayoyafanya si rahisi kwa wao wenyewe kufanya sababu
hawana uwezo wa kutosha kiuchumi kununua silaha na kujenga maficho ambayo
serikali imeshindwa kutambua kwa haraka.
No comments:
Post a Comment