Mkataba wa muda,umesitisha vita Gaza ndani ya saa tano
Baada ya mapigano makali yaliyofanyika mfululizo siku tano zilizopita
Palestina,Hamas,na Israel zimeamua kusitisha mapigano baada ya makubaliano
waliyokubaliana juu ya kusitisha mapigano makali katika ukanda wa Gaza.
Licha ya taarifa zilizotolewa jana na Israel ikiwataka
wakazi wa gaza kuhama makazi yao haraka kutokana na mashambulizi watakayo
yafanya imekubali kusitisha mashambulizi hayo kwa muda wa saa tano kutokana na
ombi lililotoka umoja wa mataifa
Shambulizi lilofanywa na Israel jana ukanda wa Gaza |
Umoja wa mataifa uliomba jeshi la Israel isitishe
mashambulizi kwa muda wa saa tano kati ya saa nne asubuhi hadi saa tisa mchana ili wananchi wanaokaa
Gaza wapate nafasi ya kupata huduma mbali mbali ikiwa pamoja na kupata chakula.
Kwa upande wa Hamas msemaji wao mkuu Sami Abu Zukhri amethibitisha kuwa na
wao watasitisha mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel wakati huo.Kutokana na makubaliano hayo toka
pande hizo mbili wameamua kusitisha mashambulizi pande zote mbili ili kuruhusu
wananchi wa Gaza wapate nafasi ya kutafuta vyakula na hudumna nyinginezo.
Msemaji wa shirika la umoja wa mataifa linalowasaidia
wakimbizi wa Palestina Christopher Gunnes amesema kuwa anamatumaini kwamba
kutokana na saa tano walizokubaliana kusitisha mashambulizi itasaidia wakimbizi
hao kupata fursa ya kusuluhisha matatizo yanayoikabili Gaza.
Jana watoto wanne wa kipalestina kutoka familia moja walipoteza
maisha kutokana na shambulizi la mizinga lililofanywa na Israel watoto hao
walipatwa na umauti wakati wakicheza katika ufuo wa bahari huko Gaza,kitendo
hiki kilizidi kuongeza jazba kwa wapalestina.
Mama wa watoto wanne waliokufa jana kutokana na shambulizi la mizinga liliofanya na Israel katika ufuo wa Gaza akiomboleza. |
Kutokana na mkasa huo wa Israel kuwaua watoto wasio na
hatia,Israel ilijitetea na kudai kuwa hawakuwa na lengo la kuua watoto hao nia
yao ilikuwa ni kuendeleza mashambulizi kwa wapiganaji wa Hamas hivyo basi vifo
vya watoto hao vilitokana na mkasa mkubwa wa mapigano hayo.
Hadi sasa Israel imesababisha vifo vya mamia ya wapalestina
ndani ya siku tano mfululizo,licha ya mazungumzo yanayoendelea ya kuleta amani gaza bado viongozi wa Hamas hawaamini
kama Israel itasitisha mashambulizi kauli hiyo ilisemwa na msemaji wa Hamas
Osama Hamdan.
wapalestina walionusurika baada ya shambulizi la mizinga toka israel jana |
Rais wa Marekani Barrack Obama amezidi kuiunga mkono Israel
na kusema kuwa Israel ina haki ya kujilinda.
Licha ya makubaliano hayo ya kusitisha mashambulizi baina ya
pande mbili hizo,Hamas bado haijaridhia makubaliano hayo sababu hoja zao
hazijatiliwa maanani hadi sasa.
No comments:
Post a Comment