Rais Goodluck Jonathan aomba msaadawa bilioni moja ili kununua vifaa vya kuikabili Boko Haram
Serikali ya Nigeria imeomba msaada wa bilioni moja ili
kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram ambao wamesababisha janga kubwa katika
Taifa hilo mwaka huu.
Rais Jonathan alituma barua katika bunge la seneti ili
kuidhinisha ombi hilo ambalo litasaidia kuimarisha vifaa vya kijeshi.
Watu zaidi ya 2,000 wamepoteza maisha na damu nyingi
imemwagika kutokana na mashambulizi yaliyosababishwa na kundi hilo,Rais
Goodluck Jonathan amezidi kupewa shinikizo ili atafute suluhu ya kundi hilo
kutokana na uharibifu unaoendelea kufanywa na Boko Haram.
Baadhi ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram linaloitikisa nchi ya Nigeria |
Jeshi la Nigeria lina upungufu mkubwa wa vifaa vya
kijeshi ambavyo vingeweza kusaidia
kupambana na wanamgambo hao,ingawa jeshi hilo halijatoa tamko rasmi kama lina
upungufu wa vifaa hali harisi inaonyesha dhahiri kwamba inahitajika msaada
mkubwa wa vifaa ili kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram.
Rais Goodluck Jonatha alidai kuwa kuna umuhimu wa
kuliongezea jeshi hilo vifaa vya kivita ili liweze kukabiliana na kundi la
Boko Haram,kundi hilo hivi karibu lilitoa tishio kwa serikali ya Jonathan na
kusema kuwa lipo njiani kuandaa mashambulizi mengine.
Wananchi wengi walitoa hoja zao pamoja na maoni baada ya
serikali kutoa tamko kwamba kuna upungufu wa vifaa wengi wao walisema kwamba
jeshi hilo limezidi kutumia vibaya rasilimali zilizopo ikiwemo na vifaa vya
kivita.
No comments:
Post a Comment