Tunisia imesema kuwa takribani wanajeshi 14 wameuawa na
wengine 20 wamejeruhiwa katika shambulizi la wanamgambo karibu na mpaka wa
Algeria.
Wanajeshi wa Tunisia |
Mashambulizi hayo yalifanywa na kundi la Okba Ben Nafaa
Brigade ambalo linasadikika kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la
Al-Qaeda,kundi hilo lilifanya mashambulizi wakati wa mgharibi ambapo wanajeshi
hao walikuwa wanafuturu.
Jeshi la Tunisia limekuwa likitekeleza oparesheni yake
katika eneo hilo ili kujaribu kuwatimua wanamgambo wanaojificha katika eneo
hilo,toka mwaka jana nchi ya Tunisia ilianza kuweka jeshi lake katika mlima huo
ili kuwazuia wanamgambo wasiweke kambi.
Serikali ya Tunisia imetangaza siku tatu mfululizo za
maombolezo kuanzia leo ,matukio kadhaa kama haya yalisha wahi kutokea mwaka
2013
No comments:
Post a Comment