Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,John Kerry
amewasili Israel na kuwataka waache mapigano.
Lengo la kuwasili waziri huyo nchini Israel ni kusaidia
mchakato wa kupata maridhiano ya amani baina ya waisrael na wapalestina.
Waziri John Kerry ameungana na katibu mkuu wa umoja wa
mataifa Ban Ki Moon kutoa tamko la usitishwaji wa uhasama kati ya pande hizo
mbili zilizokuwa mahasimu kwa muda mrefu.
Israel ilianza mashambulizi mwezi julai tarehe 8 baada ya
Gaza kuanzisha mashambulizi ya roketi Israel.
No comments:
Post a Comment