Wednesday, 23 July 2014

Ubaguzi wa rangi katika soka ukomeshwe



Mchezaji katika mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 wa klabu ya Manchester  amelazimika kutoka nje ya uwanja katika mechi ya kirafiki kutokana na kitendo cha unyanyasaji na ubaguzi wa rangi.
Mfaransa huyo mweusi Seko Fonana (19)alipatwa na mkasa huo wakati timu yake ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Croatia,mmoja kati ya wachezaji wa timu ya Croatia alimbagua kutokana na rangi yake.
Mchezaji wa Manchester Seko Fonana
Tofauti ya rangi imezidi kushika kasi katika nyanja mbali mbali hasa katika soka ambapo wachezaji weusi wamekuwa wakikumbwa na mkasa wa kubagulia wawapo uwanjani sababu ya rangi yao.
Manchester City imesema mchezaji huyo alibaguliwa na mchezaji wa timu ya Croatia,hivi karibuni wakati wakicheza mechi ya kirafiki.
Katika michuano ya kombe la Dunia shirikisho la soka ulimwenguni lilianza kuchukua hatua za kibinadamu dhidi ya mashabiki wanaotumia itikadi za rangi kubagua watu weusi kwa kuwaadabisha mashabiki wa timu ya Mexico ambao walifanya kosa kama hilo la ubaguzi wa rangi.

No comments: