Thursday, 17 July 2014

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Hague atangaza kujiuzulu

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alisema  jumatatu kuwa anajiuzulu kama mwanadiplomasia wa juu baada ya miaka minne katika kazi hiyo, ikiwa ni sehemu ya  mabadiliko makubwa yaliofanywa na waziri mkuu David Cameron tangu kuchaguliwa kwake 2010.
Waziri William Hague

Hague aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba anajiuzulu na hatagombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Mei mwakani.Vyombo vya habari vya Uingereza vinasema nafasi yake huenda ikachukuliwa na Phillip Hammond waziri wa sasa wa Ulinzi.
Mkuu wao  Bw.Cameron ambaye ni kiongozi wa chama cha Conservative anafanya kile kinachotarajiwa kuwa mabadiliko ya mwisho ya baraza lake la mawaziri  kabla ya uchaguzi huo mkuu wa kitaifa. Anatarajiwa kutangaza majina kadhaa ya mawaziri wapya Jumanne.      

No comments: